Friday, November 7, 2014

KEKI RAHISI

Vipimo
Siagi                     Kikombe 1
Sukari                   Kikombe 1 
Unga                     Vikombe 2 
Maziwa                  1/2 (nusu) Kikombe 
Mayai                    4
Baking Powder      1 Kijiko cha supu
Arki rose                kidogo
Tupike Sote sasa
1.                      Washa mkaa wako au kama unatumia  oveni 350 - 400 Deg C liache lishike moto huku ukitayarisha mchanganyiko wa keki.
2.         Changanya sukari na siagi mpaka ichanganyike.
3.                       Mimina mayai na maziwa uchanganye vizuri.
4.                       Mimina Baking Powder kwenye unga na uchanganye vitu vyote pamoja na arki rose.
5.                       Endelea kuchanganya vizuri mpaka uhakikishe vimechanganyika vizuri (unaweza kufanya bila ya mashine)
6.                       Chukua trey  yenye umbo upendalo ambayo haitojaa ukiimimina, ipake siagi na umimine mchanganyiko wako. Trey isiwe nzito sana au nyepesi sana bali iwe wastani.
7.                       Ipike (Bake ) mpaka iwive.kama unatumia mkaa moto chini kiasi na juu kiasi ili isiungue.
8.        Epua iache ipoe ndio ukate kate vipande. 


No comments:

Post a Comment