Monday, November 3, 2014

KINYWAJI CHA NDIZI NA MAZIWA ( BANANA MILK SHAKE)
Ndizi                                                 2
Maziwa vikombe                              2
Vikjiko  vya Asali/Sukari                 2
Vipande vya barafu                           8
Limao/Ndimu                                    1

JINSI YA KUANDAA
·         Osha ndizi vizuri,menya katakata weka kwenye blender
·         Mimina na vitu vyote vilivyobakia(Maziwa,asali,barafu na Limao)
·         Saga mpaka itoe kitu kama povu
·         Mimina katika glass tayari kwa kunywa


N.B
Kama hauna vipande vya barafu,saga alafu weka katika fridge unywe baada ya kupata baridi kiasi.

FAIDA ZAKE.
- Inapunguza hatari ya magonjwa ya moyo,kisukari na pressure. 
- Inasaidia kumeng’enya chakula 
- Inaondoa msongo wa mawazo 
- Inapunguza maumivu wakati wa hedhi 
- Ina madini mengi ya Pottasium na Iron 
- Inaongeza uwezo wa kufikiri 
- Inaongeza nguvu mwilini 
- Inapunguza maumivu ya vidonda vya tumbo.


Ahsante,
Rahma Chuma./Image by Fauzia M. Afif


No comments:

Post a Comment