Tuesday, November 24, 2015

JINSI YA KUTENGENEZA BREAD ROLLS STEP BY STEP

Amazing Dinner Rolls
24 Rolls
Mahitaji
  • Maji ya uvuguvugu kikombe 1
  • Backing powder  vijiko 2
  • Robo kikombe sukari nyeupe
  • Kikombe kimoja maziwa ya uvuguvugu
  • Kikombe kidogo blueband
  • Yai moja 
  • Chumvi kijiko cha chai 1
  • Unga wa ngano kilo 1





  • Jinsi ya Kuandaa

    Changanya Blueband na sukari kama unataka kupika cake,alafu tia maziwa na yai,endelea kuchanganya.
    Tia chumvi endelea kukoroga,alafu tia unga wako kidogo kidogo endelea kukoroga,alafu tia maji anza kukanda kwa mikono.Alafu.....fuatilia picha.




















Chef Rehema Chuma.

Thursday, November 13, 2014


MAHITAJI
Tangawizi fresh 1
Maji masafi vikombe 2
sukari kijiko 1
chocolate/cocoa


                                         

                                           1.Menya tangawizi uioshe alafu uikwaruze
                                             chemsha kwenye maji yemye sukari mpaka yachemke vizuri
                                              chuja kwenye kikombe chako.


                                     
                                          2.Weka Cocoa yako kiasi ukipendacho,na kama ukiona kahawa kali                                                          waweza ongeza maji ya moto kiasi (dilute)








                                               3.Kunywa kahawa yako fresh.




FAIDA ZAKE



                 Inapunguza Blood Pressure (BP)

                Inaondoa maumivu wakati wa hedhi.

                Inasaidia Mmeng'enyo wa chakula

               Inaondoa kichefu chefu na kutapika
       
                 Inapunguza kubana kifua (Asthmatic Attack)
     
                 Inafungua koo lilioziba na inaondoa kikohozi

                Inapunguza Chorestrol 

                Inapunguza hatari ya kansa ya kizazi


                Inaondoa maumivu ya misuli



By
Chef Rehema Chuma.

          


.









Friday, November 7, 2014

KEKI RAHISI

Vipimo
Siagi                     Kikombe 1
Sukari                   Kikombe 1 
Unga                     Vikombe 2 
Maziwa                  1/2 (nusu) Kikombe 
Mayai                    4
Baking Powder      1 Kijiko cha supu
Arki rose                kidogo
Tupike Sote sasa
1.                      Washa mkaa wako au kama unatumia  oveni 350 - 400 Deg C liache lishike moto huku ukitayarisha mchanganyiko wa keki.
2.         Changanya sukari na siagi mpaka ichanganyike.
3.                       Mimina mayai na maziwa uchanganye vizuri.
4.                       Mimina Baking Powder kwenye unga na uchanganye vitu vyote pamoja na arki rose.
5.                       Endelea kuchanganya vizuri mpaka uhakikishe vimechanganyika vizuri (unaweza kufanya bila ya mashine)
6.                       Chukua trey  yenye umbo upendalo ambayo haitojaa ukiimimina, ipake siagi na umimine mchanganyiko wako. Trey isiwe nzito sana au nyepesi sana bali iwe wastani.
7.                       Ipike (Bake ) mpaka iwive.kama unatumia mkaa moto chini kiasi na juu kiasi ili isiungue.
8.        Epua iache ipoe ndio ukate kate vipande. 


Monday, November 3, 2014

KINYWAJI CHA NDIZI NA MAZIWA ( BANANA MILK SHAKE)
Ndizi                                                 2
Maziwa vikombe                              2
Vikjiko  vya Asali/Sukari                 2
Vipande vya barafu                           8
Limao/Ndimu                                    1

JINSI YA KUANDAA
·         Osha ndizi vizuri,menya katakata weka kwenye blender
·         Mimina na vitu vyote vilivyobakia(Maziwa,asali,barafu na Limao)
·         Saga mpaka itoe kitu kama povu
·         Mimina katika glass tayari kwa kunywa


N.B
Kama hauna vipande vya barafu,saga alafu weka katika fridge unywe baada ya kupata baridi kiasi.

FAIDA ZAKE.
- Inapunguza hatari ya magonjwa ya moyo,kisukari na pressure. 
- Inasaidia kumeng’enya chakula 
- Inaondoa msongo wa mawazo 
- Inapunguza maumivu wakati wa hedhi 
- Ina madini mengi ya Pottasium na Iron 
- Inaongeza uwezo wa kufikiri 
- Inaongeza nguvu mwilini 
- Inapunguza maumivu ya vidonda vya tumbo.


Ahsante,
Rahma Chuma./Image by Fauzia M. Afif


Wednesday, August 28, 2013

ALHAMDULILLAH!!!!1

ALHAMDULLILAH,
Blogger wenu mnamo tarehe 05.08.2013,niliripoti sehemu yangu mpya ya kazi.
Kila siku ALLAH atenda miujiza katika maisha yangu.

Wednesday, July 24, 2013

KUFUTURISHA SASA NI FASHION KWA WASANII WETU!!!

Hivi Jamani sasa hivi kufuturisha ni FASHION au KULIPA KISASI...Mana anaefuturisha  na wanao futurishwa sidhani kama wanachunga mapenzi ya ALLAH katika zoezi hilo...Dah...INNA LILAH WA INNA ILAH RAJIUN!!!

Friday, March 15, 2013